Shirikisho la Soka nchini TFF limesikitishwa na utaratibu uliotumiwa na Uongozi wa Shule ya Gilbert Bayi wa kudai stahiki zake kupitia vyombo za habari.

TFF muda mchache uliopita wametoa taarifa ya kusikitishwa huko, na kuisambaza kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Taasisi hiyo ya Soka nchini imekiri kudaiwa fedha zaidi ya Milioni 70, baada ya kupunguza deni la zaidi ya shilingi milioni 500.

Mapema hii leo taarifa za Uongozi wa Shule ya Filbert Bayi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, baada ya mahojiano yaliyofanywa na kituo cha ITV.

Taatifa hiyo ilieleza: Uongozi wa Shule za Filbert Bayi umetishia kulishitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baada ya kushindwa kulipa deni la zaidi ya shilingi milioni 76 lililotokana na mkataba wa kutoa huduma za viwanja, chakula, malazi na usafiri kwa timu za taifa za vijana na wanawake zilizoweka kambi katika shule hiyo iliyopo Kibaha kuanzia Machi 6, 2019 kwa gharama ya shilingi milioni mia tano ishirini na moja laki nne na hamsini na tano.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 21, 2021
Kiongozi wa mpito Mali anusurika kuchomwa kisu