Awali kulikuwa na taarifa kwamba Mwamuzi Martin Saanya na msaidizi wake namba moja, Samuel Mpenzu, kwenye mechi ya Oktoba Mosi iliyomalizika kwa sare ya 1-1 kati ya Yanga na Simba, wamefungiwa miaka miwili baada ya kuboronga mtanange huo wa watani wa jadi.
Taarifa iliyotolewa Jana na TFF, Waamuzi hao bado hawajafungiwa  na Kamati ya Bodi ya Ligi ya uendeshaji na Usimamizi wa Ligi iliyokaa juzi, imefikia uamuzi wa kuendelea kujiridhisha kwa kuangalia ulivyokuwa uchezeshaji wao.
Uamuzi huo, maana yake watatu hao hawajewa adhabu hadi hapo kamati itakapojirisha na kutoa taarifa.
Taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo, zimeeleza, baada ya kujiridhisha kupitia kamishna wa mechi, inaweza kurejea na kulizungumzia hilo suala.
kilichoamuliwa jana na kamati, lakini taarifa zimeanza kuzagaa kila sehemu.
Baada ya kulikwepa Rungu mpaka sasa, Saanya, kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya facebook (pichani chini) amechapisha taarifa iliyotolewa na kamati kwa vyombo vya habari na kuisindikiza na ujumbe ‘I just Keep quiet!’ akimaanisha anakaa kimya.
Maneno hayo huenda ni kibehi kwa watu wanaosema vibaya kuwa amefungiwa, ingawa bado anachunguzwa na tayari kadi nyekundu aliyotoa kwa  Nahodha wa Simba, Jonas Mkude, imefutwa.

Mkakati Wa Ukodishaji Waiva, Bodi Ya Wadhamini Yaweka Mguu Sawa
DC Mtaturu awapa wiki moja viongozi wa vijiji kusoma mapato na matumizi