Shirikisho la soka nchini (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusu suala la beki Hassan Kessy kuwa sehemu ya kikosi cha yanga wakati wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Toto Africans waliokubali kufungwa mabao 2-0.

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema Yanga walikua sahihi kumtumia Kessy kwani hoja ya Simba ni kwamba mchezaji huyo alivunja mkataba baada ya kusaini kwa mabingwa hao huku akiwa bado na Mkataba na vinara wa ligi na sio pingamizi la usajili.

“Kuna minong’ono kuwa Yanga watakatwa pointi kwa kumchezesha Kessy hiyo habari sio kweli, Simba inadai beki huyo alivunja mkataba ila hawakuweka pingamizi kwenye usajili wake kwahiyo ni sahihi kuendelea kuwatumikia mabingwa hao huku suala lake likiendelea kushughulikiwa,” amesema Lucas.

Kwa mujibu wa mkataba wa Simba na beki huyo, Kessy anatakiwa kuilipa Simba dola 600,000 kwa kuvunja mkataba ambapo TFF limezitaka pande zote kukutana haraka kumaliza suala hilo.

Tanzia: Mwanamuziki nguli Achieng Abura afariki dunia
TASWA Kuongoza Kongamano La Mabadiliko Simba, Yanga