Shirikisho la soka nchini TFF  limetangaza viingilio vya mchezo wa ‘Watani wa Jadi’ Simba na Young Africans  wa ligi kuu soka Tanzania bara utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi Octoba mosi.
Simba inakutana na watani wao wakiwa vinara wa ligi baada ya kushinda Michezo mitano na kutoka sare mmoja huku Yanga wakishinda minne, kutoka sare mmoja na kupoteza mmoja.
Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amevitaja viingilio hivyo kuwa VIP A ni sh 30,000 VIP B & C sh 20,000 na mzunguko utakuwa sh 7,000.
Mashabiki watakaotaka kushuhudia mtanange huo uwanjani watatakiwa kutumia tiketi za Kielectoniki ambazo ndiyo pekee zitakazowezesha kuutazama mchezo huo ambao unaziba mianya yote ya kuingia bila kulipa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Selecom ambao ndiyo wasimamizi wa tiketi hizo Galus Runyeta alisema tiketi hizo zitaanza kuuzwa kuanzia kesho katika vituo mbali mbali jijini hapa.
Baadhi ya vituo hivyo ni Vituo vya mafuta vya Total, Village Supermarket, Vituo vya mafuta ya Puma, Samaki Samaki, Buguruni Sheli, Mlimani City, Sinza Africa Sana na Uwanja wa Taifa.

Aidha Galus amewataka mashabiki wa timu hizo kununua tiketi mapema kuanzia kesho katika vituo tajwa ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza siku ya mtanange huo.

Wenger Amkingia Kifua Sam Allardyce
Waataalam wa ndege wampongeza JPM, wamshauri jinsi ya kuifufua ATCL na kuwabana mafisadi