Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Chabanga Hassan Dyamwale (76).

Amesema kuwa mbali ya kuwa mtendaji ambaye alifanya mabadiliko makubwa katika soka la Tanzania kutoka ligi ya kituo kimoja hadi ligi ya mikondo miwili (nyumbani na ugenini), amesema kuwa alifanya kazi hiyo akiwa kwenye hema.

“Nimeguswa sana na kifo cha Mzee Chabanga Hassan Dyamwale, natuma salamu zangu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, majirani na marafiki wa hayati Mzee Dyamwale ambaye nimetaarifiwa kuwa amefariki dunia Agosti 13 mwaka huu,” amesema Karia.

Hata hivyo, ameongeza kuwa atamkumbuka zaidi hayati Dyamwale kwa uhodari wake wa kazi na msimamo kwenye jambo aliloliamini, na kuleta mafanikio makubwa katika soka la Tanzania.

 

Joselu Akaribia Kutua St James' Park
Kenyatta amjibu Raila kuhusu mgomo wa kwenda kazini