Katika kuonyesha mshikamano uliopo kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Kaimu Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Linah George Mwakyembe, mke wa  Dkt. Harrison Mwakyembe.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Linah amefariki katika dunia katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwaajili ya kupatiwa matibabu.

“Hakika nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Linah ambaye ambacho kimetokea katika Hospitali ya Aga Khan, Kifo hiki kimeleta huzuni kubwa kwa wanafamilia ya michezo hususani mpira wa miguu, natuma salamu za rambirambi kwako Mheshimiwa Waziri wetu mpendwa, hakika nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huu, ni pigo kubwa katika familia, ndugu, jamaa na marafiki hawana budi kuwa watulivu na wenye subira,” amesema Karia.

Hata hivyo, ameongeza kuwa anaungana na familia ya Dkt. Mwakyembe katika msiba huo ambao pia ni msiba wa wanafamilia ya michezo hapa nchini kwakuwa ni Waziri mwenye dhanmana ya kuongoza michezo.

JPM atuma salamu za rambirambi kwa Dkt. Mwakyembe
Giroud atikisa nyavu Arsenal iking'ara Australia

Comments

comments