Shirikisho la soka nchini TFF, limezikumbusha klabu za Ligi Kuu Ya Soka Tanzania Bara, Ligi Daraja La Kwanza na Ligi Daraja La Pili ambazo hazijafanya usajili kupitia mfumo wa usajili wa TFF FIFA Connect kufanya usajili wao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mchana huu na ofisi ya katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, imeeleza kuwa wamebaini baadhi ya klabu za ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili bado hazijafanya usajili kupitia mfumo huo mpya, hali ambayo huenda ikahatarisha mpango wa kutumika kwa wachezaji ambao hawatatambuliwa kwenye mfumo wa usajili wa TFF FIFA Connect.
Taarifa hizo zimesisitiza kuwa, klabu ambazo hazifanya hivyo, bado zina nafasi ya kukamilisha utarabu wa usajili, na kama viongozi wao wameshindwa kufuatia changamoto za kimtandao, wamombwa kuwasiliana na  shirikisho hilo, ili kupata msaada wa kukamilisha mapungufu yaliyojitokeza, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili juma hili.
Msisitizo mwingine uliotolewa na TFF kwa klabu ambayo itashindwa kufanya usajili kwa mfumo huo maalum, itakua na kila sababu ya kutoshiriki ligi husika msimu wa 2018/19, na ikiwezekana itashushwa daraja.

Dirisha la Usajili linatarajiwa kufungwa siku ya Alhamis Julai 26,2018 na tayari TFF imeshasisitiza hakutakuwa na muda wa ziada katika usajili wa kipindi hiki.

Vilabu ambavyo havijafanya usajili kupitia mfumo wa TFF FIFA Connect mpaka sasa

LIGI KUU:
Ruvu Shooting,Mbeya City,Tanzania Prisons,Mtibwa Sugar,Mwadui,Kagera Sugar,Alliance,Lipuli,African Lyon,KMC na Azam
Ligi Daraja La Kwanza (FDL):
Ashanti United, Boma FC, Friends Rangers, Green Warriors, Kiluvya United, Majimaji FC, Mashujaa FC, Mawenzi Market, Mbeya Kwanza, Mgambo Shooting, Njombe Mji, Pamba FC, Dar City na Polisi Tanzania
Ligi Daraja La Kwanza (SDL):
Area C United, Changanyikeni, Cosmopolitan FC, Kumuyange FC, Gipco FC, Mirambo FC, Madini FC, Mkamba Rangers, Mvuvumwa, Polisi Dar, The Mighty Elephant, Toto African, Villa Squad, Majimaji Rangers, Mtwivila City, Kasulu Red Star na Sahare All Stars
Chelsea kutenga eneo maalum
Mesut Ozil afunguka picha yake na Tayyip Erdogan

Comments

comments