Ile michezo mi tatu ya Ligi Kuu Ya Soka Tanzania Bara ya mzunguuko wa Nane Duru la Kwanza, sasa zitafanyika kesho Jumatano Novemba 9, 2016.

Michezo hiyo inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ambayo ilipewa jina la Mechi Na. 57 itachezwa Uwanja wa Mwadui wakati Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika mchezon Na. 60 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Mchezo mwingine utazikutanisha Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Uhuru jijini katika mchezo Na.59.

Michezo hiyo ilipangiwa ratiba, lakini tarehe zake hazikupangwa (TBA). Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko hayo.

Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda mjini Harare nchini Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.

Mkataba Wa Hector Bellerin Wanukia Emirates Stadium
Diego Milito Ampigia Debe Leonardo