Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), haijazuia vibali vya kukamilisha miradi ya kimkakati ya kupeleka umeme vijijini, kwa kupitisha nguzo za umeme katika hifadhi za misitu nchini.

Hayo yamebainishwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja wakati akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu aliyetaka kujua mikakati ya Serikali ya kutochelewesha vibali vya kuruhusu umeme kupita kwenye hifadhi za misitu, ili kuwahisha usambazaji huo wa umeme.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja.

Amesema, “Sheria ya Misitu Sura ya 323 haijazuia upitishaji wa nguzo za umeme katika Hifadhi za Misitu hapa nchini, kifungu cha 26 cha Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002, kimeweka utaratibu kwa anayetaka kufanya shughuli mbalimbali ndani ya Hifadhi ya Msitu.”

Hata hivyo, Naibu waziri huyo wa Maliasili na Utalii amesema TFS kwa nyakati tofauti imekuwa ikishirikisha Wizara za kisekta kukamilisha miradi ya kimkakati ya kupeleka umeme vijijini kwa wakati.

GGML yatoa mafunzo kazi kwa wahitimu vyuo vikuu
SportPesa yamuibua Jemedari Said