Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Wilaya ya Manyoni imetakiwa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kujiunga na miradi ya ufugaji nyuki ili kuendeleza uhifadhi wa mazingira na kujiongezea kipato kutokana na mazao yatokanayo na ufugaji nyuki.

Hayo, yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja wakati wa kikao na watumishi wa TFS kilichofanyika Januari 20,2023 Wilayani Manyoni, Mkoani Singida.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja.

Amesema, “‘”wajibu wenu ni kutoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi ili jamii ielewe na muwe na programu zinazooneshwa kwenye luninga kuelimisha jamii. Pia muhakikishe asilimia kubwa ya wawekezaji kwenye miradi ya ufugaji nyuki wawe ni wananchi wa kawaida ili kuwafanya wasikate miti.”

Kwa upandewake, Mhifadhi Mkuu Shamba la Nyuki Manyoni, Hashimu Gau amesema madhumuni ya kuanzisha hifadhi hiyo ni kulinda ikolojia ya Itigi ambayo ni maarufu kwa kuzalisha mazalia ya nyuki, eneo hilo pia hutumiwa na jamii kwa kutundika mizinga yao hivyo kujipatia kipato na ajira za muda mfupi za usafishaji mipaka ulinzi na usafi wa mizinga.

Sabilo akiri maji yamezidi unga Mbeya City
CCM yaibana Wizara vishikwambi vya Walimu