Klabu ya Chelsea imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Michy Batshuayi kwa kumsainisha mkataba wa miaka mitano.

Chelsea wamemsajili Batshuayi akitokea kwenye klabu ya Olympique Marseille ya nchini Ufaransa, ambayo aliitumikia tangu mwaka 2014.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, anakua mchazaji wa kwanza kusajiliwa na meneja mpya wa Chelsea, Antonio Conte kwa ada ya uhamisho inayotajwa kufikia Pauni milioni 33.

Msimu uliopita Batshuayi alifanikiwa kufunga mabao 17 na kutoa pasi za mwisho tisa akiwa na klabu ya Olympique Marseille inayoshiriki ligi ya nchini Ufaransa (Ligue 1).

Chama La Wana (Stand United) Lamnasa Adam Kingwande
Mitihani Miwili Ya Serengeti Boys Hii Hapa