Kilio cha Kanye West kuomba msaada kutokana na kusongwa na madeni kimemfikia The Game ambaye ameamua kumpa msaada wa $10,000,000 kwa masharti yaliyowekewa ‘deadline’. 

Kupitia Twitter, The Game ameeleza kuwa japokuwa yeye sio mmiliki wa Facebook ambaye Kanye alimuomba amsaidie pia, ameamua kutoa kiasi hicho cha fedha endapo rapa huyo atapanda ndege haraka na kuungana naye Dubai.

The Game ameeleza kuwa baada ya kufika Dubai, wawili hao washiriki kwenye zoezi la kuruka kutoka juu ya jengo refu au ndege iliyo angani (skydive).

The Game TweetThe Game Tweet 2

The Game alimtaka Kanye West kujibu ndani ya saa moja kwa kumpigia simu au kuandika Twitter.

Hii karibuni Kanye alitangaza kuomba msaada wa kumaliza madeni yanayomkabiri yenye thamani ya $53,000,000.

Skydive

Skydive

 

Wakurugenzi wa wanne wa halmashauri wafyekwa, wahonga wakaguzi wa CAG kuficha uchafu
Isaac Mwangi: Nitajiuzulu Kwa Muda