Rapa the Game amepigia mstari uamuzi wake wa kuachana na muziki lakini ametangaza ujio mwingine kabla ya kustaafu muziki wa rap.

The Game ambaye amekuwa akieleza kukunwa vikali na albam ya Kendrick Lamar ‘DAMN’, amepost picha akiwa na rapa huyo kwenye eneo linaloonekana kuwa ni mgahawa, na kuweka wazi kuwa ameanza kurekodi albam yake ya mwisho.

Hata hivyo, kupitia post yake ya Instagram, hakuweka wazi kama Kendrick atakuwa mmoja kati ya vichwa vitakavyosikika kwenye albam hiyo. Lamar hivi sasa anayezungumziwa zaidi ambaye albam yake imefika mauzo ya Platinum ndani ya muda mfupi.

“Excuse my eyes….. I’m high as giraffe pu*** #SaturdayNightLive Vibin’ wit my nigga @kendricklamar on this #WestSideStory shit…. to the studio to start my last album,” read the caption.” Aliandika.

Game na Kendrick Lamar wamewahi kufanya kazi pamoja mara kadhaa ikiwa ni pamoja na ‘The City’ ya mwaka 2011, “See No Evil” ya mwaka 2012 na “On Me” ya mwaka 2015.

NASA ya Raila Odinga yatishia kususia uchaguzi
Video: Rais Dkt. Magufuli asikia kilio cha wananchi Dodoma, aifuta rasmi CDA