Real Madrid wameendelea kutetea nafasi ya kuwa klabu ya soka tajiri duniani kwa mwaka nne mfululizo.

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na jarida la biashara la Forbes la nchini Marekani, klabu hiyo ya mjini Madrid nchini Hispania, imebainika kuwa na thamani wa dola za kimarekani bilioni 3.645 sawa na Pauni bilioni 2.52 za kiingereza.

Tathmini hiyo imezingatiwa mapato ya mwaka yaliyokusanywa na klabu ya Real Madrid, kwa mwaka ambapo imebainika msimu wa mwaka 2015-16 wamejikusanyia dola za kimarekani milioni 694 sawa na Pauni milioni 480 za kingereza.

Katika orodha iliyochapishwa na jariba hilo, mahasimu wakubwa wa Real Madrid huko nchini Hispania, FC Barcelona wanashika nafasi ya pili na baada ya hapo klabu za nchini England zinafuatia zikiongozwa na Manchester United.

Hata hivyo katika orodha ya klabu za michezo tajiri duniani, klabu ya Real Madrid imekamata nafasi ya pili, ikitanguliwa na klabu inayoshiriki ligi ya American Football (NFL) ya Dallas Cowboys ambayo ina utajiri wa dola za kimarekani bilioni 4 sawa na Pauni bilioni 2.77 za kiingereza.

Orodha kamili ya klabu za soka zilizopo katika kumi bora ya kuwa na utajiri mkubwa duniani msimu wa 2015-16, kwa mujibu wa jarida la Forbes.

  1. Real Madrid – US$3.645 bn (£2.52billion)
  2. Barcelona – $3.549bn (£2.46bn)
  3. Manchester United – $3.317bn (£2.3bn)
  4. Bayern Munich- $2.678bn (£1.85bn)
  5. Arsenal – $2.017bn (£1.4bn)
  6. Manchester City – $1.921bn (£1.33bn)
  7. Chelsea – $1.661bn (£1.15bn)
  8. Liverpool – $1.548bn (£1.07bn)
  9. Juventus- $1.299bn (£900million)
  10. Tottenham – $1.017bn (£704m)

 

Muhimu: US – Dola za kimerakani, bn – bilioni, m – Milioni, £ – Pauni za kiingereza.

Diamond, Mafikizolo watua Bungeni
Mahakama yaamuru Tigo kuwalipa AY, FA mabilioni kwa kutumia nyimbo zao bila idhini

Comments

comments