Vanessa Mdee amekuwa msanii wa kwanza Tanzania kupokea Plaque ya ‘Nyota Wa Mchezo’ baada ya kutajwa kama ‘Nyota wa Mchezo’ mwishoni mwa mwaka jana kwenye vipengele vya  #BestFemaleAct #BestPerformer #BestLiveAct #EmergingArtistOfTheYear.

Plaque hiyo inatolewa na kipindi cha The Playlist cha Times Fm na mtangazaji Omary Tambwe aka Lil Ommy kwa kutambua mchango na mafanikio ya msanii na kazi nzuri aliyozofanya.

Kwa mujibu wa Lil Ommy, lengo la Plaque hiyo ni kuwapa nguvu na kusherehekea mafanikio ya kazi za msanii na sanaa kwa ujumla Tanzania.

“Wazo la kumtambua na kumtunuku ‘Nyota wa Mchezo’ lilianza Disemaba mwaka jana ambapo nilitumia twitter kutaja wasanii wengi kama ‘Nyota wa Mchezo’ kuwatambua walifanya vizuri kwenye sanaa ya muziki wa kizazi kipya,” amesema Lil Ommy.

“Vanessa alikuwa mtu wa kwanza kuandika tweet yake na wazo lilianzia baada ya kumfikiria yeye na kuona kazi nzuri alizofanya na baadae nikaendeleza orodha ya watu wengi kwa hashtag ya #BongoFleva2017 #NyotawaMchezo na kutaja nafasi zao (vipengele) ambavyo wamefanya vizuri,” ameongeza.

Mtangazaji huyo ameeleza kuwa aliangalia impact (matokeo/athari) ya msanii, impact ya kazi zake, popularity (umaarufu), kujulikana, airplays (kazi yake kuchezwa kwenye radio na TV), views (watazamani kwenye YouTube), anavyozungumziwa kwenye mitandao ya kijamii, ubora wa kazi, ukuaji wa msanii, ukomavu wa msanii na kuwataja kama NYOTA WA MCHEZO.

Amesema Januari 22 mwaka huu (jana) alim-surprise Vanessa Mdee baada ya kufanya naye mahojiano maalum wakiichambua albam yake ya kwanza na ‘nzito’ ya Money Mondays, kisha kufanya makabidhiano maalum ya Plaque hiyo kutokana na kazi yake.

Naye Vee Money alionesha furaha yake kwa plaque hiyo kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram, akiitaja Jumatatu kama siku yake nzuri zaidi.

“Asanteni Sana Sana Sana…Leo nimezawadiwa tuzo ya Playlist Nyota wa Mchezo 2017. #BestFemaleAct #BestPerformer #BestLiveAct #EmergingArtistOfTheYear.

“Mondays are my FAVORITES ? just received a plaque from @timesfmtz Playlist MVP of the year 2017. Asante Sana @lilommy ??? album link in my bio,” Vee ameandika kwenye Instagram.


Lil Ommy ambaye anatajwa kuwa mmoja kati ya watangazaji watano waliofanya vizuri zaidi mwaka jana, amesema lengo lake ni kuhamasisha kiwanda cha burudani Tanzania kutambua kazi za wasanii na kusapoti sanii yetu kama kiwanda kinachotoa ajira kwa vijana na kuchangia pato la Taifa. Aliongeza Lil Ommy.

Netanyahu amshukuru Trump kwa maamuzi ya Kihistoria
Chama cha SPD chataka kuanza upya mazungumzo na CDU na CSU