Mshambuliaji kutoka nchini England na klabu ya Arsenal, Theo Walcott yu njiani kuondoka kaskazini mwa jijini London na kuhamia magharibi mwa jiji hilo yalipo makao makuu ya klabu ya West Ham Utd.

Walcott yu tayari kuachana na Arsenal, mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuchoshwa na mpango wa meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger wa kumtumia kama mchezaji wa akiba.

Tayari amzungumzo ya awali kati ya mchezaji huyo na uongozi wa The Gunners yameshafanyika juu ya kutarajia kuondoka kwake mwishoni mwa msimu huu, na sasa kinachosubiriwa ni kutumwa kwa ofa ya klabu ambayo itakuwa tayari kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Klabu ya West Ham Utd, imekua ya kwanza kuonyesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili Walcott, kufuatia mipango iliyowekwa hadharani na wawekezaji klabuni hapo David Gold na David Sullivan ya kuandaa ofa ya kufanya usajiali wa mshambuliaji mwenye uzoefu na ligi ya nchini England, kama walivyoagizwa na meneja wao Slaven Bilic.

Uongozi wa klabu hiyo unaamini Walcott, ni mchezaji mwenye vigezo vinavyotakiwa na meneja huyo kutoka nchini Croatia, na atakapowasili huko magharibi mwa jijini London atawasidia kufikia lengo la kufanya vizuri zaidi, tofauti na ilivyokua msimu huu.

West Ham Utd, pia imeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Olympic Marseille Michy Batshuayi pamoja na mshambuliaji wa klabu ya  Olympic Lyon Alexandre Lacazette.

Pia yupo mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan, Mauro Icardi ambaye pia anawaniwa na klabu za Man Utd pamoja na Chelsea.

11 Wa Kwanza Dhidi Ya Yanga Hawa Hapa
KAMPUNI YA KIJAPAN KUWEKEZA KWENYE UMEME