Jina la mlinda mlango chaguo la kwanza kwenye timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) Francis Uzoho, limeondolewa kwenye kikosi cha wachezaji watakaokabiliwa na jukumu la kupambana na kupata ushindi katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika 2019 dhidi ya Afrika kusini, Novemba 17.

Uzoho anayeitumikia klabu ya Elche inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania, amelazimika kuondolewa kwenye kikosi cha Super Eagles, kufuatia majeraha ya mbavu yanayomkabili kwa sasa.

Taarifa zilizotolewa na uongozi wa klabu yake, zinaeleza kuwa, mlinda mlango huyo ambaye aliitumikia Nigeria wakati wa fainali za kombe la dunia mwaka huu 2018, huenda akawa tayari kucheza tena soka, baada ya majuma manne.

Hii ni mara ya kwanza kwa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 20 kukosekana kwenye kikosi cha Nigeria, tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza, Mwezi Novemba mwaka 2017, kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Argentina.

Tayari kocha mkuu wa Super Eagles Gernot Rohr ameshatangaza kujaza nafasi ya Uzoho, kwa kumuita mlinda mlango wa klabu ya Enyimba Theophilus Afelokhai.

Image result for Theophilus AfelokhaiMlinda mlango wa klabu ya Enyimba Theophilus Afelokhai.

Mbali na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afika 2019 dhidi ya Afrika kusini, Super Eagles itacheza mchezo mwingine wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uganda Novemba 20, kwenye uwanja wa Keshi mjini Asaba.

Kikosi kilichotajwa kwa ajili ya michezo hiyo:

Makipa: Theophilus Afelokhai (Enyimba); Ikechukwu Ezenwa (Enyimba) na Daniel Akpeyi (Chippa United, South Africa)

Mabeki: Olaoluwa Aina (Torino, Italy); Adeleye Aniyikaye (FC IfeanyiUbah); Semi Ajayi (Rotherham United, England); Bryan Idowu (Lokomotiv Moscow, Russia); William Ekong (Udinese, Italy); Leon Balogun (Brighton & Hove Albion, England); Kenneth Omeruo (Leganes, Spain) na Jamilu Collins (SC Padeborn, Germany)

Viungo: Oghenekaro Etebo (Stoke City, England); John Ogu (Hapoel Be’er Sheva, Israel) na Mikel Agu (Vitoria Setubal, Portugal)

Washambuliaji: Ahmed Musa (Al Nasr, Saudi Arabia); Kelechi Iheanacho (Leicester City, England); Moses Simon (Levante, Spain); Victor Osimhen (Royal Charleroi SC, Belgium); Odion Ighalo (Changchun Yatai, China); Alex Iwobi (Arsenal, England); Samuel Kalu (Bordeaux, France); Isaac Success (Watford, England); Samuel Chukwueze (Villarreal, Spain)

Wachezaji wanaosubiri endapo kutatokea dharura: Henry Onyekuru (Galatasaray, Turkey); Chidozie Awaziem (Porto, Portugal); Nyima Nwagua (Kano Pillars); Sunday Adetunji (Enyimba) na Junior Lokosa (Kano Pillars)

Prof. Mbarawa atoa onyo kali kwa watendaji wa mamlaka za maji
Live Dodoma: Mkakati na mpango kazi wa kujumuisha masuala ya jinsia ndani ya Bunge

Comments

comments