Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ametangaza mipango ya kuongeza vitega uchumi barani Afrika baada ya nchi yake kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Ametoa ahadi hiyo akiwa nchini Afrika Kusini, ambapo ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya barani Afrika

Akihutubia kwenye bunge la Afrika Kusini jijini Cape Town, May ameahidi dola bilioni 5.1 kusaidia uchumi wa nchi za Afrika ili nchi hizo ziweze kutenga nafasi za ajira kwa ajili ya vijana.

May pia ameahidi kuleta mabadiliko ya kimsingi katika utaratibu wa kutoa misaada utakaozingatia changamoto za kiuchumi na kiusalama za muda mrefu kwa lengo la kupunguza umasikini barani Afrika.

Aidha, katika ziara yake barani Afrika anatarajia kujadili namna Uingereza itakavyoendeleza na kuimarisha ushirikiano huo pamoja na Afrika ili kuongeza vitega uchumi na hivyo kudumisha utulivu na usalama.

Hata hivyo, Waziri Mkuu May ameongeza kuwa, miongoni mwa nchi tajiri duniani za kundi la  G7, anataka Uingereza iwe ya kwanza katika uwekezaji vitega uchumi barani Afrika hadi utakapofika mwaka 2022.

 

Esma auponda wimbo wa Hamisa adai aache kuomboleza
Ronaldo de Lima atarudi Hispania?