Waziri Mkuu wa Uingereza ameshindwa vibaya katika kura ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya – maarufu kama Brexit – katika bunge la Uingereza baada ya wabunge kupinga mswaada wake kwa kura 432 kwa 202.

Mara baada ya kipigo hicho, May amesema kuwa kutokana na wingi wa kura za kupinga mswaada huo serikali yake itaruhusu mswaada wa kutokuwa na imani kujadiliwa bungeni.

Aidha, wakati anarudi kukaa chini, kiongozi wa chama cha upinzani cha Leba, Jeremy Corbyn mara moja alithibitisha kuwa amewasilisha kura ya kutokuwa na imani na serikali ya May, mswaada ambao utajadiliwa Jumatano.

Hata hivyo, May alikuwa amewasilisha mbele ya bunge mpango mzima wa jinsi Uingereza itakavyojitoa katika Umoja wa Ulaya suala ambalo liliidhihirishwa katika kura ya maoni mwaka 2016.

LIVE: Rais Magufuli akipokea hati za utambulisho wa Mabalozi
Video: Ugaidi tena Kenya, Magufuli akerwa atoa tamko zito