Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ameweka hadharani ushauri aliopewa na Rais wa Marekani Donald Trump wakiwa wawili, kuhusu mchakato wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, ushauri aliodai ni ‘ukatili’.

Akizungumza na BBC hivi karibuni, May alisema kuwa Trump alimshauri kuachana na mchakato wa kufanya mazungumzo ya makubaliano na Umoja wa Ulaya badala yake aufungulie mashtaka umoja huo.

“Aliniambia ninapaswa kuuburuza mahakamani Umoja wa Ulaya, na kutoendelea kufanya nao makubaliano mezani,” alisema May.

Juni 23, 2016 asilimia 51.9 ya wananchi wa Uingereza waliopiga kura kuhusu mpango wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya uliopewa jina la Brexit waliunga mkono mpango huo, kinyume na ushawishi wa Waziri Mkuu huyo.

Kwa mujibu wa sheria za Umoja wa Ulaya, Uingereza inaweza kujiondoa kwenye umoja huo kuanzia Machi mwakani na sio mapema zaidi.

Hata hivyo, Uingereza imelazimika kukaa mezani na kufanya mazungumzo na Umoja huo kuhusu namna itakavyoishi ikiwa nje yake. Masuala yanayoleta utata zaidi ni pamoja na namna ya kufanya biashara na nchi za umoja huo hupo baadaye, dhidi ya sheria na masharti yake.

Hata hivyo, Theresa May alirejea kauli yake na kudai kuwa ingawa Trump alikuwa anamsihi kutoendelea na mazungumzo, wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari jijini London ni kama alimuona akimaanisha “usiondoke kwenye meza ya mazungumzo.”

Trump alitembelea Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu huyo pamoja na Malkia Elizabeth II.

Maelfu ya waandamanaji wanaopinga sera za Trump pamoja na uwepo wake ndani ya nchi hiyo waliifunga baadhi ya mitaa, lakini haikumzuia kiongozi huyo wa Marekani kukamilisha ziara yake kwa utulivu na kisha kuelekea Scotland kwa mapumziko ya siku mbili akiwa na mkewe.

Polepole: Hatuna wasiwasi, tutapata ushindi mkubwa kwa sababu ya kazi nzuri
Said Fella aanika mshahara anaolipwa na Diamond