Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, anajiandaa kuwasilisha ombi kwa Umoja wa Ulaya la kucheleweshwa kwa angalau miezi kadhaa, kwa Uingereza kujiondoa katika muungano huo ili kuuwezesha mchakato huo kuendelea kwa utaratibu.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya bunge la Uingereza wiki iliyopita kupiga kura mara mbili kuyakataa mapendekezo ya May, huku Spika wa bunge hilo, John Bercow akiamuru kwamba wabunge hawangeendelea kupiga kura kwa hoja ambayo walikuwa wameikataa mara mbili mfululizo.

Aidha, karibu miaka mitatu sasa imepita tangu Waingereza wapige kura ya azma ya kujiondoa katika muungano wa umoja wa nchi za ulaya, unaoundwa na mataifa 28 barani humo.

Msemaji wa waziri mkuu wa nchi hiyo, Theresa May amesema kuwa huenda Waziri huyo akawasilisha barua ya kutaka kuongezewa muda siku ya Jumatano kwa rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk.

Hata hivyo, wachambuzi wanasema kuwa ni vigumu kubashiri nini itakuwa hatima ya mvutano huo unaoendelea Uingereza na iwapo Uingereza itajitenga kama ilivyokusudiwa kwa kura ya mwaka 2016.

Kimbunga Idai chaleta maafa, magari ya misaada yakwama
CUF yazidi kupukutika, wengine 11 watimkia CCM