Mlinda mlango wa klabu ya Chelsea, Thibaut Courtois amepanga kumfikishia ujumbe meneja mpya wa klabu hiyo, Antonio Conte kwa kumuarifu juu ya mipango yake ya kutaka kuondoka endapo uongozi wa utashindwa kumtimizia haja zake.

Courtois, amekua katika shinikizo la kuutaka uongozi wa klabu ya Chelsea kufanyanae mazungumzo ya kusaini mkataba mpya ambao utajumuisha mambo yake ya msingi katika utendaji wake wa kazi za kila siku huko Stamford Bridge.

Mlinda mlango huyo kutoka nchini Ublegiji, amekua akipata wakati mgumu wa kukamilishiwa mpango huo, kutokana na viongozi wa Chelsea, kulichukua suala hilo kama nila kawaida, hali ambayo imeonyesha kumkera Courtois.

Tayari Courtois, ameshautaka uongozi wa The Blues kumbadilishia kocha wa makipa, baada ya kukiri kutofurahishwa na huduma anayopatiwa na Christophe Lollichon aliyedumu klabuni hapo kwa kipindi cha miaka 10.

Pia kipa huyo mwenye umri wa miaka 24, amekiri kusikitishwa na kutopendezwa na msimu wa 2015-16 ambao unaelekea ukingoni huku The Blues wakishindwa kuwa sehemu ya timu zitakazoshiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Hata hivyo tayari Courtois, ambaye alipelekwa kwa mkopo tangu mwaka 2011 kabla ya kurejea mwaka 2014, anahushwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ya Real Madrid, hali ambayo inazidisha uchochezi wa kuondoka kwake klabuni hapo.

Kama itatokea Courtois anaondoka Stamford Bridge, wakati wa dirisha la usajili, Antonio Conte hatokua na njia nyingine zaidi ya kumtumia mlinda mlango atakaesalia Asmir Begovic kama chaguo lake la kwanza.

Rais Magufuli atua kwa Museveni
Antonio Conte Apigania Kumbakisha Eden Hazard