Winga wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Monaco, Thomas Lemar aliyekuwa akitafutwa na klabu kubwa za ligi kuu ya Uingereza amefikia makubaliano ya awali ya kujiunga na klabu ya Atletico Madrid.

Ada ya paundi milioni 65 ni kiasi kinachotajwa kutolewa na Atletico Madrid ili kufanikisha uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye ameitumikia Monaco kwa miaka mitatu akitokea katika klabu ya Caen.

Miongoni mwa klabu za ligi kuu nchini Uingereza zilizokuwa zikimsaka mchezaji huyo ni pamoja na Arsenal na Liverpool ambapo Liverpool walikuwa tayari kutoa kitita cha paundi milioni 60 kumpata mchezaji huyo.

Katika michezo 123 alizoichezea klabu ya Monaco, Lemar amefunga mabao 22 katika na aliwasaidia kushinda ligi kuu ya Ufaransa ‘Ligue 1’ na kufika nusufainali ligi ya klabu bingwa Ulaya msimu wa 2016-17 huku katika timu ya taifa ya Ufaransa akiwa tayari amefunga mabao matatu katika mechi 12 alizowachezea tangu mwaka 2016.

 

DK. Shika: Naingiza viwanda 30 nchini vya uwekezaji, 'Tutaelewana tu'
Video: Nape akubali lawama ya 'Bao la mkono', JPM awapasha viongozi wa dini