Washika bunduki wa Ashburton Grove (Arsenal), wameonyesha dhamira ya dhati ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa pembeni wa mabingwa wa soka nchini Ufaransa AS Monaco Thomas Lemar.

Arsenal wameripotiwa kutuma ofa ya Pauni Milioni 35 ambayo wanaamini itawezesha mchakato wa kuanzishwa kwa mzungumzo ya usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

Dhamira ya usajili wa Lemar imekuja, kufuatia uwezekano wa The Gunners kushindwa kuafikiana na mshambuliaji wao wa pembeni kutoka nchini Chile Alexis Sanchez ambaye bado hajasaini mkataba mpya.

Mkataba wa Sanchez utafikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao, na kwa kuhofia asiondoke kama mchezaji huru, Arsenal huenda wakamuweka sokoni katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Awali Arsenal walituma ofa ya Pauni milioni 28 kwa ajili ya usajiliwa Lemar, lakini viongozi wa AS Monaco waliiweka kapuni baada ya kuona haina thamani.

Katika hatua nyingine meneja wa Arsenel Arsene Wenger anatajwa kukaribia kuvunja rekodi ya usajili ndani ya klabu hiyo, kufutia mpango wa kuhitaji huduma ya mshambuliaji wa Olympic Lyon Alexandre Lacazette ambaye thamani yake inatajwa kufikia Pauni milioni 57.

Rekodi ya usajili ghali ndani ya klabu ya ya Arsenal iliwekwa na jkiungo mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil aliposajiliwa kwa Pauni Milioni 42.5 mwaka akitokea kwa mabingwa wa Hispania Real Madrid.

Video: 'Tumechoka matapeli, sasa Serikali tumeamua tufike' - Rais Magufuli
Tanzania yailalamikia Kenya kupiga marufuku uuzwaji wa Gesi