Bayern Munich wamepata ushindi wao wa 4 katika hatua ya makundi ya Champions League msimu huu – lakini usiku wa Jumanne pia ilikuwa ni siku ya Thomas Muller kuandika rekodi mpya na kuwazidi Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Raul.

Muller alifunga goli la 3 la Bayern katika ushindi wa 4-0 vs Olympiakos lakini pia ushindi wa leo pia ulikuwa ni wa 50 kwa kiungo mshambuliaji huyo wa kijerumani katika ligi ya mabingwa wa ulaya.

Muller ameweka rekodi ya kuwa mwanasoka mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutimiza idadi ya mechi 50 za ushindi katika Champions League – ametimiza idadi hiyo akiwa na miaka 26 na siku 72.
Raul alitimza idadi hiyo akiwa na umri wa miaka 26 na siku 257 hivyo Muller ameivunja rekodi hiyo.

Alichokisema Papa Francis Baada ya Kutua Kenya
Dani Alves Amchongea Cristiano Ronaldo