Kocha wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund, Thomas Tuchel ameripotiwa kuwa amekataa nafasi ya kuwa kocha mkuu wa Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu kwa kile kinachodaiwa anatarajia kujiunga na klabu ya Arsenal.

Thomas Tuchel (44) amekuwa hana kazi tangu afukuzwe kuifundisha Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu uliopita, amekuwa akihusishwa na taarifa za kuchukua nafasi ya Jupp Heynckes ndani ya klabu ya Bayern Munich.

Hata hivyo Tuchel inasemekana lengo lake ni kufundisha timu ambayo ipo nje ya ujerumani kwa mara ya kwanza na tayari ameshaanza mazungumzo na klabu ya Arsenal.

Tuchel anaonekana kuwa na asilimia kubwa ya kuchukua nafasi ya Arsene Wenger, ambaye  huenda akaondoka ndani ya timu hiyo ambayo ameifundisha kwa Zaidi ya miaka 20.

Aidha, Arsene Wenger kwa kipindi kirefu amekuwa akikabiriwa na shinikizo la kutakiwa kuachia nafasi ya kuifundisha timu hiyo kutoka kwa mashabiki na wengi wanaamini msimu huu huenda ukawa wa mwisho kwa kocha huyo ndani ya Arsenal.

EAEO: Idadi kubwa ya wahitimu vyuoni hawana sifa za kuajiriwa
Video: ''Anachofanya Ebitoke ni cha kawaida sana'' Blackpass