Katika kuitikia wito uliotolewa wa Rais Dkt. John Magufuli, wa kuwataka watuhumiwa wa uhujumu uchumi kutubu na kurudisha fedha za Serikali, Mbunge wa Muleba Kaskazini, Anna Tibaijuka ameahidi kurejesha fedha alizopokea kutoka kwa mtuhumiwa wa uhujumu uchumi, James Rugemalira, bilioni 1.6 kwaajili ya kujengea bweni la shule.

Prof, Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba kaskazini (CCM) amesema suala la kurudisha fedha siyo lake binafsi bali bodi ya shule Barbro Johanson ndiyo iliyokaa kikao na kuafikia kurudisha fedha hizo ili kulipa deni la James Rugemalira ambaye ni mtuhumiwa wa uhujumu uchumi.

” fedha ni za shule lakini mwenyekiti Solomoni Udungana na wazazi wamekaa kwenye kikao na kuamua kwamba fedha zirudi na mimi nimeshukuru kwa msimamo huo kwasababu ndiyo msimamo wangu binafsi” amesema Prof. Tibaijuka.

Amesema kuwa licha ya kua fedha hizo walizopewa na Rugemalira zilitumika kujenga bweni la shule, taasisi hiyo itatafuta fedha sehemu nyingine na kumlipia ili aachiwe huru.

Aidha amebainisha kuwa kwa upande wa Rugemalira yeye bado hajapewa taarifa za uamuzi huo wa shule ya Barbro Johanson kumrejeshea fedha alizowapa.

 

Video: TAKUKURU kumulika ujenzi machinjio ya Vingunguti
Video: DC Mjema aagiza polisi 'kuwagonga Dada Poa', Radi yaua wanne wakinywa pombe