Mwimbaji TID aka Mnyama kama anavyopenda kuitwa, ametishia kutinga katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Quick Rocka na kundi la OMG.

TID ambaye ana historia ya kufikishwa yeye kwenye kituo ha polisi na hata kufungwa miezi kadhaa, sasa amebadili upepo na yeye anahitaji haki yake kisheria.

Kupitia mtandao wa Instagram, Mnyama ametishia kufika polisi kuwasilisha malalamiko yake kutokana na kile alichodai kundi la OMG na Bosi wao Quick wametumia wimbo wake ‘Watasema’ bila ruhusa yake. Hivyo, anahitaji kulipwa angalau milioni 20 kama kifuta jasho kwa kazi yake iliyowahi kushinda tuzo mbili.

“Wat is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka & @omgtanzania we need to TALK #Watasema, ameandia msanii huyo. Naomba tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 inKenya u can’t just Steal it, Unalala Ndani Leo.” ameandika TID.

‘Watasema’ ni hit ya miaka mingi iliyopita, ambapo TID alimshirikisha Naaziz, malkia wa michano kutoka Necessary Noise ya Kenya.

Lowassa aimulika ‘kamatakamata’ viongozi wa Chadema, asema imetosha
Sigara yasababisha watu 123 kuteketea kwa moto