Muigizaji Tiffany Haddishi aliyesababisha mitandao iwake moto wa aina yake baada ya kudai kuwa Beyonce alimwambia kuna mrembo ambaye alimng’ata usoni, huku akificha jina lake ameamua kusema neno la mwisho kuhusu sakata hilo.

Tangu Tiffany alipokaririwa akieleza jinsi ambavyo Beyonce alimsimulia tukio hilo la kung’atwa usoni, mitandao ya kijamii ililipuka kwa hashtag ya kutaka kujua nani aliyekuwa na ujasiri wa kumng’ata mwimbaji huyo usoni #whobitbeyonce kwa takribani wiki nzima.

Jumatano, Tiffany aliamua kutumia mtandao wa Instagram akiwa mubashara kwa video na kuwashushua wanaotumia muda mwingi kutaka kumjua aliyemng’ata Beyonce, huku akidai kuwa kuna mambo mengi ya msingi wangepaswa kuyafanya na kuachana kupoteza muda kwa udaku huo.

“Watu wanapaswa kujikita kwenye masuala ya msingi yaliyopo, kama vile kulipa kodi. Kwa sababu muda wa kulipa kodi kwa watu wengi umefika sasa. Ni muda wa kujiuliza Je, watoto wako wanajua kusoma na kuandika? Nyumba yako ni safi?,” alihoji.

“Hayo ndiyo masuala ya kujikita kwayo sasa. Lakini kila mtu anahangaika sasa kujua aliyemng’ata Beyonce. Hiyo siyo habari ya muhimu. Nitawaambia neno la mwisho na sitazungumzia tena hili,” aliongeza.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 38 amesema kuwa Beyonce alimsainisha makubaliano ya kutotoa siri ya aliyemng’ata, kwa lugha ya kigeni ‘Non-Disclosure Agreement (NDA)’. Hivyo, hatasema kuhusu hilo.

Chombo cha Anga cha China chapoteza mwelekeo, sasa kutua Duniani siku ya Pasaka
Urusi yajibu mapigo ya Marekani, yawafukuza Wanadiplomasia 60

Comments

comments