Mlinda mlango wa kutumainiwa nchini Marekani Tim Howard huenda akakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne, kufuatia jeraha alilolipata akiwa katika majukumu ya kuitumikia timu ya taifa lake.

Taarifa za kuumia kwa mlinda mlango huyo ambaye aliwahi kuwa tegemeo la klabu ya Everton ya nchini England, zimetolewa na klabu yake ya sasa ya Colorado inayoshiriki ligi ya nchini Marekani (MLS).

Howard alipatwa na majeraha ya kuchanika nyama za paja la mguu wake wa kulia, akiwa katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia ukanda wa Amerika ya kati na kaskazini, ambapo kikosi cha timu ya taifa ya Marekani kilikubali kichapo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya Mexico.

Kufuatia taarifa hizo, tayari Tim Howard ameshaondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Marekani, ambacho hii leo kitashuka tena dimbani kucheza mchezo mwingine wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Costa Rica.

Uongozi wa klabu ya Colorado umeeleza kuwa, mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 37, atafanyiwa upasuaji siku la Al-khamis mjini Los Angeles.

Frank Lampard Kuondoka Marekani
Wayne Rooney Aumia, Hatarini Kuikosa Arsenal