Mlinda mlango wa klabu ya Newcastle, Tim Krul atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha msimu wa 2015-16 kilichosalia baada ya kupata majeraha akiwa na timu yake ya taifa ya Uholanzi.

Krul, aliumia goti wakati wa mchezo wa kuania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016, dhidi ya Kazakhstan waliokubali kichapo cha mabao mawili kwa moja.

Jana daktari wa timu ya taifa ya Uhoanzi alithibitisha kuumia kwa mlinda mlango huyo, baada ya kumfanyia vipimo na imebainika hatoweza kucheza katika kipindi cha msimu kilichosalia.

Krul, aliumia goti katika dakika ya 81 ya mchezo huo na ililazimika kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na malinda mlango wa akiba na kumaklizia mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Astana.

Krul anatarajiwa kurejea Tyneside, nchini England kwa ajili ya kuendelea na matibabu

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 27, amekua nguzo muhimu katika lango la Newcastle Utd, na hivyo itamlazimu meneja wa klabu hiyo Steve McClaren, kumrejesha mlinda mlango Freddie Woodman aliyekua akiitumikia klabu ya Crawley Town kwa mkopo.

Ulazima wa kurejeshwa kwa mlinda mlango huyo kutoka nchini England, unatokana na mlinda mlango chaguo la pili huko St James’ Park, Karl Darlow kuwa majeruhi katika kipindi hiki.

CCM Wajibu, ‘Kama Watakubali Matokeo Iwapo Watashindwa’
Prezzo Wa Kenya Ampa Sapoti Magufuli