Mwimbaji Justin Timberlake ameweka wazi taharuki iliyowakuta yeye na mwenza wake, Jessica Biel dakika chache baada ya kuingia katika chumba cha kujifungulia hospitalini, mwaka 2015.

Mkali huyo wa RnB aliliambia jarida la Entertainment Tonight kuwa walikuwa wamejiandaa na kuhakikishiwa na madaktari kuwa mke wake angejifungua kwa njia ya kawaida, lakini dakika chache kabla mambo yalibadilika na akatakiwa kufanyiwa upasuaji.

Alieleza kuwa mkewe alifanyiwa upasuaji wa dharura uliofanikisha kumpata mtoto wao wa kiume, Silas.

“Tuliporudi nyumbani tulikuwa tumechoka, tumechanganyikiwa lakini pia tulikuwa na taharuki,” alisema Timberland.

 

Video: Usione Simba kalala ukamchezea sharubu- JPM, Maandamano kutikisa ukuta Mererani
Mahakama yaamuru Anudo Ocheng arejeshwe Tanzania