Times FM Radio ya jijini Dar es Salaam, leo inatarajia kuzindua rasmi msimu wake mpya wa kipindi cha The Playlist.

Kipindi hicho kilichokuwa kikirushwa kupitia 100.5 Times Fm kila Jumamosi sasa kitaanza rasmi kurushwa mara tano kwa wiki, kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni.

Mtangazaji wa The Playlist, Omary Tambwe maarufu kama Lil Ommy ameiambia Dar24 kuwa watu wengi maarufu wamealikwa na watafanyiwa mahojiano.

“Katika uzinduzi wa leo kutakuwa na suprise nyingi kwa sababu tumewaalika mastaa kibao waliowahi kubonyeza ngoma tano kwenye The Playlist ambao wataenda hewani moja kwa moja wakati hafla fupi ya kinyamwezi ikiendelea,” amesema Lil Ommy.

Kipindi hicho kinachoongozwa na Omary  Tambwe maarufu kama Lil Ommy hualika watu maarufu na kufanya nao mahojiano.

Katika hatua nyingine, Times Fm wamezindua nembo yao mpya inayoashiria muonekano mpya na ratiba mpya ya vipindi vyake.

Utulivu watawala nchini Kenya kuelekea uchaguzi mkuu
Lulu ataja kinachozimaliza filamu za kitanzania