Timu ya taifa ya Saud Arabia imenusurika kupata ajali mara baada ya Ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji hao  kuelekea kusini mwa Urusi, kwa ajili ya kuendelea na michuano ya kombe la dunia kupata hitilafu katika moja ya injini yake.

Picha za video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaionyesha ndege hiyo chini ya bawa lake kukiwa na cheche za moto.

Aidha, Ndege hiyo ya shirika la Rossiya ilipatwa na hitilafu hiyo wakati ikitua uwanja wa Rostov-on-Don kwa ajili ya kuwashusha wachezaji hao.

“Tunamshukuru Mungu,msafara mzima umefika salama, Kulikuwa na matatizo ya kiufundi, na tulipatwa na hofu kuwa,” amesema  kiungo wa Saudi Arabia Atan Bahbir

Hata hivyo, shirikisho la mpira wa miguu nchini Saudia,limesema kuwa wachezaji wote wapo salama, na wako tayari kucheza katika mchezo wao dhidi ya Uruguay hapo kesho.

 

Atletico Madrid wafanya umafia kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa
Salah awafikirisha kocha na kipa wa Urusi, ‘tutaona’

Comments

comments