Meneja wa klabu ya Corinthians Adenor Leonardo Bacchi (Tite), ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Brazil zinaeleza kwamba, Tite ataondoka klabuni hapo na kwenda kufanya shughuli za kitaifa.

Tangazo hilo liltolewa na rais wa klabu hiyo Roberto de Andrade katika mkutano na wanahabari baada ya kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha wa taifa hilo Dunga.

Dunga alifukuzwa kutoka na timu hiyo kupata matokeo mabovu na kutupwa nje ya michuano ya Copa America inayoondelea nchini Marekani.

Brazil wameshindwa kufuzu hatua ya makundi baada ya suluhu ya 0-0 dhidi ya Ecuador, ushindi wa 7-1 dhidi ya Haiti na kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Peru

Waziri Mkuu Majaliwa ameitaka Mikoa yote iunde kamati ya Amani
Video: Rais Magufuli amewatakia Waislamu wote Mfungo mwema wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani