Mwimbaji wa Nigeria, Tiwa Savage ameeleza mapito aliyopitia kwenye maisha yake ya ndoa na mumewe ambaye alikuwa meneja wake katika masuala ya muziki, Tunji ‘TeeBillz’ Balogun.

Ingawa wawili hao wamekuwa katika maisha ya furaha na mapenzi tele kwa kipindi kirefu hadi kufikia uamuzi wa kuona, Tiwa anasema kuwa ugomvi ulikuwa sehemu ya maisha hayo pia na kwamba hata siku ya kufunga ndoa waliogombana nje ya mlango wa kuingia ukumbini.

Akifunguka katika mahojiano aliyofanya na ‘E! Entertainment’, Tiwa Savage ambaye ni mwanamuziki mpya wa label ya Roc Nation ya Jay Z, alisema kuwa watu walihisi kuna kitu hakiendi sawa kati yao lakini baadae walipotezea na kuingia ukumbini wakiwa wanacheza na tabasamu lililoficha ugomvi wao.

Tiwa na mumewe 2

Tiwa Savage na Mumewe

“Tulikuwa na ugomvi kidogo nje, tulikuwa tunabisana na kila mmoja alikuwa anatukaribisha ‘karibuni bibi harusi na bwana harusi’, na tulianza kucheza kuingia ndani na alikuwa kama anaunguruma wakati kamera zinatumulika,” alisema Tiwa Savage.

Maisha ya wawili hao yemekuwa yakijaa na ‘drama’ na ugomvi unaoripotiwa mara kwa mara na vyombo vya habari, na mara kadhaa  wameripotiwa kupigana chini.

Video: Chris Brown, Wizkid wafunika jukwaani na wimbo wao mpya
Video: Mbunge anataka kupigiwa Saluti, Waziri Olenasha atoa agizo