Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimeweka wazi jumla ya fedha ambazo zimekusanywa ambapo kimesema kimefanikiwa kukusanya Sh138 milioni kwa lengo la kugharamia matibabu ya Rais wa Chama hicho, Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji.

Ambapo taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa TLS, Godwin Ngwilimi amesema kiasi hicho kimepatikana kutoka kwa watu na wadau mbalimbali walijitolea kwa hali na mali kuchangia matibabu ya Tundu Lissu.

Hata hivyo Ngwilimi ameweka bayana mchanganuo wa matumizi ya fedha hiza ambapo amesema fedha hizo zimetumika kulipia gharama za matibabu pindi Lissu alipokuwa Hospitali ya Nairobi, Leuven na visa kwa watu watatu wakiwa nchini Ubelgiji.

Aidha Ngwilimi ametoa shukuran kwa wale wote waliojitokeza kuchangia matibabu ya Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa Chadema.

Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa katika makazi yake mjini Dodoma ambapo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na usiku wa siku hiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi alikolazwa hadi Januari 6 baada ya kahamishiwa Leaven, Ubelgiji kwa mazoezi ya viungo na saikolojia.

Madereva Bodaboda wala kiapo cha uaminifu kuwalinda watoto dhidi ya mimba
Trump akerwa na Waafrika, awatolea lugha chafu