Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Godwin Ngwilimi amempongeza na kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kutekeleza matarajio ya watanzania na kuahidi kutoa ushirikiano wao kwa mahakama pale unapohitajika.

Ngwilimi ametoa kauli hiyo leo Februari mosi jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama.

Pia ameomba uwezeshaji wa rasilimali fedha katika muhimili wa mahakama ili kushughulikia changamoto zinazoikabili.

Aidha ametoa wito kwa watumishi wa mahakama, majaji, wasajili, watendaji , makarani  na watumishi wengine, mawakili, wanasheria popote walipo wanatakiwa  kutambua mwelekeo wa nchi unabadilika kwa kasi, matarajio ya wananchi , kuondokana na utamaduni wa kuendelea kufanya kazi kimazoea, kutumia fursa zilizopo ikiwamo Tehama ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Pia  kuendelea kusimamia maadili ya kitaaluma na uadilifu , hata Mungu anapenda uadilifu na imeandikwa katika vitabu vitakatifu, kulinda na kuhifadhi misingi ya kitaaluma na kujifunza kwa kufuata makosa yaliyotokea hapo nyuma

Ngwilimi ametoa  wito akisema: ” Kama sehemu ya watanzania, tusitumie mahakama vibaya, kusumbua wengine, kuonea wengine, kama sehemu ya majaribio, siyo maabara , kama jumba la kamari.

Masauni ajibu tuhuma kamatakamata ya watu kuwekwa ndani zaidi ya masaa 24
Ukata walikumba jeshi, lakosa pesa ya chakula na maji