Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua za VULI 2021 kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka.

Mkurugenzi wa Huduma za utabiri Dkt. Hamza Kabelwa amesema Utabiri huu ni kwa maeneo ya Nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini, Ukanda wa Ziwa Viktoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Dkt Kabelwa amesema, Msimu wa mvua za Vuli unatarajiwa kuanza kwa kusuasua katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Oktoba 2021 ukiwa na mtawanyiko na muendelezo usioridhisha katika maeneo mengi.

Akizungumza kuhusu athari zinazotarajiwa kujitokeza, Dkt. Kabelwa amesema upungufu wa unyevunyevu katika udongo unatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi, magonjwa ya mlipuko kutokana upungufu wa maji safi na salama, upungufu wa malisho na maji unaweza kujitokeza hali ambayo inaweza kuleta uwezekano wa kutokea migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Utabiri wa msimu wa mvua za vuli 2021 unapatikana katika ofisi zote za TMA nchini pamoja na mitandao ya mawasiliano kama vile TMA online TV, tovuti, blog, facebook na Instagram.

Edna Lema: Sijafanya maamuzi
Gwajima: Chanjo kutolewa vijijini kwa huduma ya mkoba