Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza hali mbaya ya hewa kwa siku tano kuanzia Februari 12, 2020.

Taarifa ya TMA imeitaja mikoa inayotarajia kunyesha mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ni mikoa ya Lindi, Mtwara, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Morogoro Kusini pamoja na visiwa vya Unguja, Pemba na Mafia

Februari 13, 2020 mvua kubwa itanyesha kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

Huku Februari 14, 2020 angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na Kusini mwa mkoa wa Morogoro.

Angalizo la upepo mkali na mawimbi makubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, imeeleza taarifa hiyo ya TMA.

Muuguzi wa vyeti feki atuhumiwa kuua mwanafunzi
Kiporo cha Kinana, Membe , Makamba kudumu siku saba

Comments

comments