Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imetahadharisha kutokea kwa mvua kubwa kuanzia leo hadi kesho Alhamisi Septemba 27, 2018.

Taarifa ya mamlaka hiyo, imetaja mikoa itakayoathirika na mvua hizo ni Tanga, Dar es Salaam, Pwani pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja.

Aidha, TMA imewataka wananchi wa maeneo husika kuchukua tahadhari kwa sababu mvua hizo ni kubwa kwa zaidi ya asilimia 70.

“Madhara yatakayotokana na mvua hiyo ni kutokea mafuriko katika mitaa na kusababisha msongamano wa magari na watu hivyo kuchelewesha usafirishaji hasa katika maeneo ya mjini,” imesema taarifa hiyo ya TMA

Video: Mbunge Neema Mgaya amwaga chozi ajali ya MV Nyerere
Nafasi za ajira kutoka makampuni 11 Tanzania