Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imetoa tahadhari kwa wananchi na wadau wa hali ya hewa uwepo wa vipindi vifupi vya mvua kubwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Utabiri huo umetaja mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Pwani pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba kuwepo kwa mvua kubwa za kipindi kifupi.

Ambapo mvua hizo zinatarajiwa kuendelea kunyesha mpaka jumatano ya tarehe 02.5.2018 katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Kaskazini.

Aidha Mamlaka ya Hali ya Hewa imetoa tahadhari kwa baadhi ya maeneo nchini yakiwemo, Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mara, Kagera, Geita, Mwanza, Mwanza, Simiyu na Shinyanga.

Rais Museveni akosolewa vikali na wadau wa mitandao
Mkuu wa shule mbaroni kwa ubakaji