Mamlaka ya Dawa ya Vifaa Tiba nchini ,(TMDA) imefungua mashauri 146 kutokana na watu kukiuka Sheria za mamlaka hiyo.

Hayo yameelezwa na meneja wa huduma za sheria Wakili Iskari Fute wakati akiwasilisha mada kuhusu usimamizi wa sheria ya dawa na vifaa Tiba katika kikao kazi cha uhamasishaji na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Morogoro,Dar es Saalam na Pwani.

Aidha amebainisha, TMDA imekuwa ikifuatilia kwa karibu maswala yote ya sheria na kuchukua hatua kwa watuhumiwa ikiwa ni kulinda afya ya jamii.

“Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita hadi kufikia sasa TMDA imefungua mashauri 146, lakini yaliyokwisha na watuhumiwa kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kulipa faini ni 32”amesema Fute.

Pia watuhumiwa hao waliofunguliwa mashauri baada ya TMDA kufanya kaguzi mbalimbali za kushtukiza katika maeneo tofauti ikiwa ni lengo la mamlaka kulinda afya ya jamii kupitia sheria ya Dawa na Vifaa Tiba sura ya 219.

Aidha, ameeleza msingi wa sheria ya TMDA ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Sura ya 2 ibara ya 63 (c) na 64, Ibara hizo zinaweka mamlaka ya Bunge kutunga sheria zote.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Morogoro, Anza Ndossa aliyekuwa Mgeni rasmi, amewataka Wanahabari kutumia taaluma yao kufikisha elimu pamoja na kufichua wakiukwaji wa sheria za dawa na vifaa tiba.

Wagonjwa wa Saratani KCMC wapata neema
Waziri amtumbua meneja Tanroads