Tume huru ya uchaguzi nchini Togo imemtangaza rais Faure Gnassingbe kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa baada ya kupata asimilia 72.3 za kura, huku mgombea wa upinzani na waziri mkuu wa zamani Agbeyome Kodjo alieoko katika nafasi pili kwa asilimia 18.3 akipinga matokeo hayo kwa madai kwamba kulikuwepo na wizi wa kura.

Koti ya katiba inatarajiwa kuthibitisha matokeo hayo ya uchaguzi mnamo kipindi cha wiki moja.

Rais Gnassingbe aliyewania muhula wa nne ametangazwa mshindi kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi huo, ambao ulikuwa na wagombea saba.

Agbeyome Kodjo, mshindi wa pili amepata asilimia 18. 3 za kura, na nafasi ya tatu ilishikiliwa na mpinzani mkongwe wa utawala wa Gnassingbe, Jean-Pierre fabre ambaye alipata asilimia 4.3 za kura. Wagombea wengine 4 hawakufikisha asilimia moja ya kura.

Waziri wa ajira ameliambia shirika la AFP kwamba ni kwa mara ya kwanza mgombea wa chama chao kupata ushindi kama huo, Miaka mitano iliopita rais Faure Gnassingbe alichaguliwa kwa asilimia 58.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ni kwamba watu waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 76 nukta 6. Idadi hiyo ni kubwa kuliko mwaka 2015 ambapo ilikuwa ni asilimia 60. Kwa mara ya kwanza pia matokeo yametangzwa mapema kuliko chaguzi zilizopita.Kwa ujumla uchaguzi wa juma mosi ulifanyika katika hali ya utulivu.

Magufuli uso kwa uso na Prof. Lumumba wa Kenya
Ukerewe: Uhaba wa Samaki, wananchi watakiwa kufuga nyuki