Tony Bennett ambae ni mshindi wa mara 18 wa tuzo ya Grammy ameweka rekodi mpya ya Dunia ya Guinness ya kuwa mwanamuziki mwenye umri mkubwa zaidi kuachia albamu.

Bennett ambae amefikisha umri wa miaka 95 ameachia albamu yake Oktoba 1, 2021 inayokwenda kwa jina la ‘’Love for Sale’’ akiwa amemshirikisha Lady Gaga.

Aidha Bennett na Lady Gaga wamekuwa na ushirikiano wa kimuziki tangu mwaka 2011 ambapo waliachia ngoma inayojulikana kama ‘’The Lady is a Tramp’’ na miaka mitatu baadaye wawili hao waliachia albamu inayojulikana kama “Cheek to Cheek.”

Kwa Bennett hii siyo rekodi yake ya kwanza, kulingana na mtandao wa Guinness unaohusika na utoaji wa rekodi hizo umeweka wazi kuwa Bennett anashikilia rekodi nne zaidi Duniani:

Mwanamuziki mkongwe kushika nafasi ya kwanza katika chati ya album nchini Marekani kupitia albamu yake ya ‘’Cheek to Cheek, Rekodi ya Kushika muda mrefu kati ya albamu 20 za juu za Uingereza kwa miaka 39.

Pia Bennett anashikilia rekodi ya kurekodi wimbo kwa muda mrefu na kisha kurekodi upya wimbo huohuo na msanii huyohuyo kwa mara nyingine.

Senzo: Oktoba 30 zamu ya Azam FC
Siku ya lishe kitaifa kufanyika Tabora