Mkuu wa benchi la ufundi la West Brom, Tony Pulis amekisifia kikosi cha Arsenal akisema kuwa ni kizuri kuliko cha vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea.

Kauli hiyo imekuja baada ya bao lililofungwa na straika Olivier Giroud dakika za mwisho za mchezo ambao Arsenal walikilaza kikosi hicho cha Pulis kwa bao 1-0 wakiwa kwenye uwanja wao wa Emirates.

West Brom vilevile mwezi huu walifungwa dakika za mwisho wakiwa kwenye uwanja wa Stanford Bridge na kuifanya Chelsea ifikishe mechi ya 12 katika michuano ya Ligi Kuu.

Hata hivyo licha ya kikosi hicho cha Antonio Conte kuwa mbele kwa pointi saba dhidi ya Arsenal, Pulis anaamini kuwa Arsene Wenger ndiye ana kikosi imara.

“Kama utaangalia wachezaji ambao hawakucheza leo (majuzi), na ambao hawakuwemo kikosini na ukiangalia Chelsea nadhani Arsenal ndio wana kikosi imara,” alisema kocha huyo.

“Muda wote wanakuwa na kasi na inakuwa vizuri kuwaangalia kama Chelsea watafanya nini kipindi watakapokutana nao,” aliongeza kocha huyo.

Pulis alisema kuwa pamoja na Chelsea wapo kileleni mwa Ligi Kuu itawalazimu kuongeza wachezaji wengine mwezi ujao.

Kinnah Phiri Atamba Kuibanjua Mbao FC
Majimaji FC Waivimbia Azam FC