Kocha wa klabu ya Newcastle United, Rafa Benitez ameekataa kukanusha taarifa juu ya kutaka kumsajili Fernando Torres kutoka katika klabu ya Atletico Madrid.

Akiongea na gazeti la michezo la ‘MARCA’ la Hispania, Benitez amesema hajui kitu anachofikiria Torres kwa sasa lakini anadhani anawaza kwenda sehemu nyingine japo itakuwa vigumu kutua Newcastle.

”Inafaa, lakini sidhani kama itakuwa rahisi”, alisema Benitez alipoulizwa kama angependa kumsajili Torres. Kocha huyo ameongeza kuwa wakati Torres akiwa Liverpool alikuwa bora zaidi na walipoungana katika klabu ya Chelsea aliwasaidia kushinda kombe la Europa league japo hakuwa na wakati mzuri katika klabu hiyo.

Akicheza chini ya kocha Rafa Benitez ndani ya klabu ya Liverpool Torres alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 72 katika michezo 116 aliyoichezea klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na Liverpoool mwaka 2007 akitokea Atletico madrid kabla ya kurejea tena katika klabu hiyo mwaka 2015 na tayari ameweka wazi kwamba huu ndio msimu wake wa mwisho katika klabu hiyo.

 

 

Simba yafanya mkutano wa dharura, Serikali yabariki mabadiliko
Video: Wafanyakazi DataVision wafuturu pamoja na watoto wenye Saratani Muhimbili