Klabu ya soka ya Arsenal imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wapinzani wao jijini London Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.

Katika mchezo huo ambao umepigwa kwenye uwanja wa Wembley ambao ni nyumbani kwa Tottenham bao pekee la timu hiyo limefungwa na mshambuliaji Harry Kane dakika ya 49.

Aidha, matokeo hayo yanaifanya Arsenal kuendelea kubakia katika nafasi ya sita ikiwa na alama 46 kwenye mechi 27 za ligi, huku Tottenham wakiendelea kukaa katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 52 baada ya mechi 27.

Katika mchezo wa leo, Arsenal imewachezesha wachezaji wapya waliosajiliwa kwenye dirisha dogo ambao ni Henrikh Mkhitaryan na Pierre-Emerick Aubameyang lakini wameshindwa kuisadia timu hiyo kupata ushindi.

Hata hivyo, mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane ambaye anashikilia rekodi ya mchezaji aliyefunga mabao zaidi ya 100 kwenye mechi chache zaidi za EPL, leo amefikisha mabao 23 msimu huu hivyo kuendelea kujiweka vyema kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu.

 

Baada ya kunyimwa uwanja, Yanga kukarabati uwanja wake
Simba kuikabili Gendamarie kesho