Klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza imewafungia wanachama wake wanne kwa kuhusika na hujuma ikiwemo utovu wa nidhamu katika mchezo wao uliyopita dhidi ya Yanga.

Juma lililopita, Toto Africans walikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Young Africans katika mchezo wa Ligi Kuu Bara iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba matokeo ambayo yalisababisha mgogoro ndani ya klabu hiyo.

Wanachama waliofungiwa ni John Chief Kisura, Beatus Madenge na  Adamson Kibeta Ngassa ambao wanatuhumiwa kumpora fedha Katibu wa timu hiyo ambazo zinadaiwa kuwa zilikuwa za mgawo wa mapato ya mechi hiyo.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa, Makamu Mwenyekiti,  Hamad Waziri Gao naye amesimamishwa kutokana na kuihujumu timu hiyo baada ya kutoa kauli kuwa Toto haiwezi kuifunga Young Africans huku yeye akiwa kiongozi wake.

Baada ya mchezo huo kumalizika viongozi wa Toto waligawanyika huku ikidaiwa baadhi yao walijiondoa kwenye maandalizi ya mchezo huo ambapo pia wachezaji walituhumiana kuwa kuna baadhi yao wanahujumu timu kwa kucheza chini ya kiwango.

Jonas Tiboroha Kutimkia Mkoani Shinyanga
Ni Real Madrid Vs Atletico Madrid Fainali Ya Ligi Ya Mabingwa Ulaya