Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeombwa kutoa haki kwenye madai ya klabu ya Toto Africans kufanyiwa hujuma na Kasulu Red Stars, kwa kuwachezesha ‘mamluki’ katika mchezo wa mwisho ya Ligi Daraja la Pili.

Klabu hiyo ya jijini Mwanza ambayo iliwahi kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, ilimaliza Ligi Daraja la Pili kwa kichapo cha mabao mawili kwa sifuri na kushuka Daraja hadi ngazi ya Mkoa baada ya kuambulia alama 12.

Mmoja wa viongozi wa Klabu hiyo, Beatus Madenge amesema katika mchezo huo ambao ulipigwa uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, wenyeji Kasulu Red Star waliwachezesha wachezaji ambao hawakustahili.

Amesema wachezaji wote 11 waa Kasulu Red Star walighushi kadi, huku akibainisha kuwa kadi zilizotumika zilionekana wazi kuwa na mapungufu mengi tofauti na zile zilizotolewa Shirikisho.

“Kimsingi tunaiomba Bodi ya Ligi na TFF waingilie kati na kutoa haki, haiwezekani timu inaingiza wachezaji kwa kufoji kadi, Klabu zinatumia gharama kubwa kujiendesha” alisema Mjumbe huyo wa kamati ya utendaji.

Hata hivyo Kiongozi huyo amebainisha kuwa wakati mchezo huo ukiendelea walitoa taarifa kwa mamlaka (TFF), ambapo waliambiwa kuendelea na mchezo, lakini wakiandika barua na vielelezo, jambo ambalo walilitekeleza.

Nugaz: Sisi hatufungwi
JPM ateua wakuu wa mikoa miwili